Van der Vaart nje kombe la dunia
Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal atakuwa na kikosi chake bila kupata huduma ya mchezaji Rafael van der Vaart katika fainali za kombe la dunia Brazil mwaka 2014 baada ya kuumia msuli wa nyama nyuma ya goti yaani Calf.Taarifa iliyoandikwa katika mtandao wa goal.com ni kwamba Van der Vaart aliumia wakati akifanya mazoezi jana siku ya jumanne katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Ureno na kwa sasa ametolewa kwenye kikosi hicho kitakachokwenda Brazil.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa anasubiri kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wa Uholanzi kitajwe ambacho kitakwenda Brazil lakini kutokana na matatizo ya kimwili atakosa fainali yake ya tatu za kombe la dunia tokea aanze kucheza soka baada ya mwaka 2006 na 2010 kucheza fainali hizo.
0 comments:
Post a Comment