Sunday, 25 May 2014

Madrid mabingwa UEFA 2014,ni mara yao ya 10,La Decima

Hatimaye ile ‘EL DERBI MADRILEÑO’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki ulimwenguni kote pambano la Real Madrid na Athletico Madrid fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA  imemalizika muda mfupi uliopita  kwa Madrid kuibuka na ushindi wa mbao 4-1 huko Lisbon Ureno.
Atletico Madrid waliwachokoza Madrid baada ya kuongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Diego Godin kwa kichwa dakika ya 36 akiunganisha krosi kutoka upande wa kulia.
Gareth Bale alishindwa kuokoa krosi hiyo na kipa Iker Casillas akatoka mapema langoni na kukutana na mpira uliopigwa na Godin unaelekea nyavuni. Casillas aliukimbilia mpira huo na kuuwahi kuutolea nyavuni, lakini haukutoka.
Klabu ya Atletico Madrid ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Diego Costa kuumia na kutoka nje nafasi yake ikichukuliwa na Adrian Lopez Dakika ya tisa .
Mchezo ulichezeshwa na mwamuzi  Bjorn Kuipers wa Uholanzi
Real ilicharuka dakika 10 za mwisho na kushambulia sana langoni mwa Atletico, hadi kufanikiwa kupata bao la kusawazisha licha ya kukosa kadhaa ya wazi kupitia kwa Sergio Ramos.
Katika dakika 30 za nyongeza, Gareth Bale alifunga bao la  pili dakika ya 110 na Marcelo dakika ya 118 na Cristiano Ronaldo dakika ya 120 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari na amefunga bao lake la 17 katika UEFA msimu huu.
Real walihitaji taji la 10 walilobatiza jina la  ' La Decima'  na ni la kwanza l tangu mwaka 2002  lakini awali walibeba katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000 na 2002.

0 comments:

Post a Comment