Mbeya City yaanza vizuri mashindano ya Nile Basin
Taarifa kutoka huko Khartoum, Sudan zimesema Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye Michuano ya CECAFA NILE BASIN, Mbeya City, jana wameanza vyema Masindano hayo kwa kuichapa Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 kwenye Mechi ya KUNDI B.
Kwenye Mechi hii, Bmabao ya Mbeya City yalifungwa na Paul Nonga, Mwegane Yeya na Themi Felix.
Hapo Jana, Timu ya Zanzibar, Polisi, ilichapwa mabao 3-0 na Wenyeji Al-Merreikh ya Sudan.
Kufuatia kujitoa kwa Timu 5 katika Dakika za mwisho, CECAFA iliamua kubadilisha Makundi na Ratiba ya Mashindano haya.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CECAFA,
Rogers Mulindwa, Timu zilizojitoa ni pamoja na Wageni Waalikwa maalum,
Klabu za Egypt Al Masry na.Arab Contractors.
Nyingine ni Elman ya Somalia na Klabu ya Sudan, Hey Al Arab.
Hali hiyo imefanya Timu kubakia 11 na Makundi kuwekwa kuwa Matatu.
0 comments:
Post a Comment