Makocha wa Ngorongoro Heroes na Nigeria kuzungumza kesho
MAKOCHA wa timu
za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na Nigeria (Flying Eagles), Manu
Garba wanakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati yao kwa ajili ya
mechi ya Jumapili.
Mkutano huo
utafanyika kesho (Mei 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kuanzia saa 5 kamili asubuhi
Mechi hiyo ya
kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 20 itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa 10 kamili jioni katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Fainali hizo za
19 za Afrika zitafanyika mwakani nchini Senegal zikishirikisha timu saba
zitakazofuzu kwenye mechi za mchujo, na Senegal wanaoingia moja kwa moja
kutokana na kuwa wenyeji.
Wakati
Ngorongoro Heroes leo (Mei 9 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi yake
Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Flying Eagles yenyewe muda huo huo itafanya
mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa sh.
5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
0 comments:
Post a Comment