Malinzi atuma rambirambi msiba wa kocha Mwale
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu
za rambirambi Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya
kutokana kifo cha Kocha wa timu ya Nkana FC, Masauso Mwale.
Marehemu Masauso Mwale amezikwa jana katika makaburi ya Kansenshi, Ndola ambapo alifariki kwa ajili ya gari Mei 23 akiwa anaelekea kwenye kambi ya klabu ya Nkana ili kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Sewe Sports ya Ivory coast,amefariki akiwa na miaka 51.
Amesema
amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha ghafla cha Kocha Mwale, na kuongeza
kuwa msiba huo si pigo kwa Zambia pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile ni
mfano wa kuigwa kwa makocha wazalendo waliozipatia mafanikio makubwa klabu za
Afrika.
Rais
Malinzi amemuomba Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya
Mwale, na kuitaka kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito kwao.
0 comments:
Post a Comment