Wednesday, 28 May 2014

Everton yaitikisa Manchester United,inataka kumsajili Welbeck

Klabu ya Everton inajiandaa kumsajili mchezaji wa klabu ya  Manchester United Danny Welbeck ili kuziba nafasi ya  Romelu Lukaku aliyepo Evertona kwa mkopo kutoka Chelsea.
Kwa mujibu wa mtandao wa goal.com,Everton itampoteza Lukaku, ambapo mbelgiji huyo anatarajiwa kurudi kwenye klabu yake baada ya  kuitumikia Everton kwa mkopo katika ligi kuu Uingereza ambao wanatumia uwanja wa Goodison Park.
Welbeck ambaye ametajwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa  Roy Hodgson katika timu ya Uingereza kuelekea kombe la dunia Brazil 2014 hakuonesha kiwango kizuri ndani ya utawala wa David Williama Moyes msimu ulioisha..
Mapema wiki hii mchezaji huyo alionesha wasiwasi mkubwa wa majaliwa yake ya kuendelea kuitumikia Manchester United akidai kuwa hapangwi mara kwa mara.

Ikiwa Everton watafanikiwa kumshawishi kwenda kwao ni wazi kuwa Welbeck atapata amani ili aendelee kucheza ligi kuu Uingereza.
Wachambuzi wa soka wanadai kuwa Welbeck kukosa amani kunachangiwa zaidi na ukaribu wa Nahodha wa Uholanzi Robin Vana Persie pamoja na Kocha mpya wa Klabu ya Manchester United
 Louis van Gaal.

0 comments:

Post a Comment