Mbeya City dimbani usiku huu kule Sudan.
Klabu ya Mbeya City Usiku huu, kuanzia Saa 2 , watakuwa hukoKhartoum, Sudan kucheza Mechi yao ya Pili ya KUNDI B ya Mashindano ya CECAFA NILE BASIN dhidi ya Wakongwe wa Kenya AFC Leopards wakati wenzao wa Zanzibar, Polisi, Jana walichapwa mabao 3-0 na Malakia ya South Sudan.Hicho ni kichapo cha Pili kwa Polisi baada pia kupigwa 3-0 na Al Merreikh ya Sudan na hivyo wapo nje ya Mashindano na Jumanne watacheza Mechi ya kukamilisha Ratiba ya Kundi lao dhidi ya Victoria University ya Uganda ambayo Jana iliwabana Wenyeji Al Merreikh kwa Sare ya 0-0.
Matokeo hayo ya Jana yamezifanya Al Merreikh, Malakia na Victoria University kusonga Robo Fainali kutoka KUNDI A huku Kocha wa Al Merreikh, Martin Otto Pfister, akikiri Victoria University ni Timu ngumu iliyojengeka kimkakati.
Mechi ya Leo kati ya Mbeya City na AFC Leopards inazikutanisha Timu zilizoshinda Mechi zao za Kwanza kwa Mbeya City kuichapa Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 na AFC Leopards kuipiga Etincelles ya Rwanda Bao 2-0
Mbeya City watacheza Mechi yao ya mwisho ya KUNDI B hapo Jumatano dhidi ya Enticelles.

0 comments:
Post a Comment