Mbeya city yapigwa na AFC Leopards.
Mbeya City jana Usiku imefungwa mabao 2-1 na AFC Leopards ya Kenya katika Mechi yao ya Pili ya KUNDI B la Mashindano ya CECAFA NILE BASIN CUP iliyochezwa huko Khartoum, Sudan.
Hadi Mapumziko, Mbeya City walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mudde Musa katika Dakika ya 30 na Were Paul, Dakika ya 35.
Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke katika Dakika za Majeruhi.
Kwenye Mechi ya Kwanza, Mbeya City
waliifunga Academie Tchite ya Burundi mabao 3-2 na Mechi yao ya mwisho ya
KUNDI B ni hapo Jumatano dhidi ya Enticelles ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment