Mvella aula ndani ya TFF
Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania, TFF imesema kuwa Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Iringa (IRFA),
Eliud Mvella amejiunga na Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya
rais wake, Jamal Malinzi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mvella Amejiunga na Sekretarieti ya TFF katika Idara ya Sheria na Vyama Wanachama kuanzia leo (Mei 21 mwaka huu) ambapo atashughulikia masuala ya wanachama.
Mvella alijiuzulu rasmi wadhifa wake IRFA jana (Mei 20 mwaka huu). Mwenyekiti wa IRFA, Cyprian Kwihyava amepokea barua ya kujiuzulu huko ambapo ameelezea masikitiko yake kwa uamuzi huo wa Mvella.

Ni imani ya TFF kuwa Mvella atatumia uzoefu wake wa
muda mrefu katika uongozi wa mpira wa miguu kuhakikisha TFF inaimarisha
uhusiano wake na wanachama wake.
TFF ina wanachama 44 ambao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

0 comments:
Post a Comment