Real na Athletico Madrid washitakiwa na UEFA
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA imewafungulia Mashitaka Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone na Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso kwa kuwatuhumu kufanya Utovu wa Nidhamu kwenye Fainali ya ligi hiyo ya mabingwa ulaya iliyochezwa Jumamosi iliyopita huko Lisbon, Ureno na Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 4-1.
Wote hao wawili wameshitakiwa kwa makosa ya kuvamia Uwanja.
Mara mbili Diego Simeone aliingia
Uwanjani wakati wa Dakika za Nyongeza 30 kwenda kumkabili Beki wa Real
Raphael Varane na ikabidi azuiwe na Wasaidizi wake.
Pia Simeone alionyesha kukasirishwa na Refa Bjorn Kuipers wa Uholanzi.
Nae Xabi Alonso, ambaye alikosa kucheza
Fainali hiyo kwa sababu alikuwa Kifungoni, alionekana akikimbia nje ya
Uwanja baada ya Mechi hiyo.
UEFA imetamka kuwa Kesi za wawili hao
zitasikilizwa hapo Julai 17 na wakipatikana na hatia baadhi ya Adhabu
zao ni kuzikosa Mechi za UEFA Msimu ujao.
Vile vile, UEFA imezifungulia Mashitaka
Klabu zote mbili, Real Madrid na Atletico Madrid, kwa kuzoa Kadi za
Njano 5 kila moja katika Fainali hiyo.
Kwenye Mechi hiyo, Wachezaji 7 wa Atletico na 5 wa Real walipewa Kadi za Njano.
0 comments:
Post a Comment