Thursday, 22 May 2014

Suarez hatihati kucheza kombe la dunia

Mchezaji Luis Suarez anaweza kukosa Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuelezwa atakwenda kufanyiwa upasuaji baada ya Kuumia goti mazoezini jana.
Mshindi huyo wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa PFA baada ya kazi nzuri aliyoifanya msimu huu akiwa na Liverpool - ndiye tegemeo la mabao la Uruguay lakini anatakiwa nje ya Uwanja kati ya wiki nne hadj sita.
Taarifa ya FA ya Uruguay imesema: "Haikutarajiwa kabisa. taarIfa mpya ni kwamba, tumeamua cha kufanya, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kufanyiwa upasuaji.
"Hatuwezi kusema zaidi. AUF (Shirikisho la Soka Uruguay) litatangaza rasmi Alhamisi asubuhi.’
Timu hiyo ya Amerika Kusini in a mtihani mgumu katika kundi lake ilikopangwa pamoja na kikosi cha Roy Hodgson sambamba na Italia na Costa Rica.
Suarez alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari wa Uruguay jana baada ya kuumia mazoezini ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Brazil.
Jambo zuri kuhusu Suarez ni kwamba anaweza kupona ndani ya wiki nne hadi sita, lakini ikiwa kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kinatakiwa kuwasilishwa Juni 2, inaiweka katika mgumu mno nchi hiyo.
Uamuzi wowote wa kumjumuisha Suarez kikosini akiwa hayuko fiti itakuwa na kujitoa mhanga.
Hali kama hii ilimtokea Fernando Torres wa Hispania kabla ya Fainali za Kombe la dunia mwaka 2010 alipokwenda kufanyiwa upasuaji Aprili na akakaa nje kwa wiki saba. Pamoja na hayo, wakala wa mchezaji huyo ameiambia CNN anatarajiwa atakuwa fiti

0 comments:

Post a Comment