Thursday, 22 May 2014

Van Gaal ana kazi nzito-Scholes.

Kiungo Mashuhuri aliyestaafu wa Manchester United, Paul Scholes, amesema kocha mpya wa miamba hao wa Uingereza, Luis Van Gaal, anakibarua ‘kigumu zaidi’ mikononi mwake kufufua hadhi ya timu hiyo.
Scholes aliendelea kusema kuwa ikiwa wasimamizi wakuu wa timu hiyo wana nia na ari ya kurejesha mabingwa hao  kileleni kama ilivyo kuwa itikadi yao hadi kampeni iliyoisha juzi lazima wajizatiti sana.
Alizidi kunena kuwa kiungo wa kati wa Bayern Munich, Toni Kroos, ndiye anayefaa kusainiwa na van Gaal kwanza katika harakati za kujenga upya kikosi cha washindi hao mara 20 wa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza walioshuka hadi nafasi ya saba msimu huu.
“Ametumikia vilabu kubwa duniani lakini ana kazi ya ziada hapa Man United mikononi mwake.
“Itakuwa pengo kubwa kujaza ili kushika Manchester City, Chelsea na Liverpool msimu ujao. United wako nyuma sana. Van Gaal akiwaongoza kufuzu ligi ya mabingwa itakuwa ni mwanzo,” alisema Scholes.
Naibu mwenyekiti mtendaji Ed Woodward, alikuwa mshawishi mkuu kumleta van Gaal kufuatia kufutwa kwa David Moyes kama meneja lakini Scholes aliongeza hata yeye ana jukumu la kujidhihirisha kwenye msimu huu wa kiangazi.
“Kazi ni kwake kuonyesha ana uwezo wa kushawishi wachezaji wakuu wajiunge na timu hii ikiwa ana weledi wa kazi yake,” kiungo huyo aliyestaafu misimu miwili iliyopita baada ya kutumikia na kushinda mataji kocho kocho na timu hiyo alisema.

0 comments:

Post a Comment