Vidic kucheza mechi ya mwisho leo Old Traford.
Nahodha wa klabu ya
Manchester United, Nemanja Vidic anatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho Old
Trafford wakati kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na Ryan Giggs
kitakapoikaribisha Hull City katika mchezo wao wa mwisho nyumbani kwa msimu huu
leo jioni.
Vidic mwenye umri wa
miaka 32 amekuwa mmoja wa mabeki bora wa Ligi Kuu toka asajiliwe United mwaka
2006 lakini nyota huyo wa kimataifa wa Serbia atajiunga na Inter Milan majira
ya kiangazi baada ya kukataa kuongeza mkataba.
Beki huyo wa kati
amecheza zaidi ya mechi 300 katika kipindi cha miaka nane aliyokuwa Old
Trafford akishinda mataji matano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka
2008.
Vidic amesema hajutii
uamuzi wake wa kuondoka kwani amekuwa akicheza kwa uwezo wake wote katika
kipindi cha miaka nane aliyokuwepo na anadhani huo ni wakati muafaka wa
kuondoka.
0 comments:
Post a Comment