Uchaguzi wa Simba ni Juni 29,fomu kuanza kutolewa keshokutwa
MEI 7,2014
Uchaguzi mkuu wa Simba SC sasa umepangwa kufanyika Juni
29 mwaka huu baada ya tarehe iliyokuwa imepangwa awali Mei 3 mwaka huu
kupanguliwa baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo na Klabu kukataa
kuipitisha Katiba ya klabu hiyo iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo makao makuu ya Simba SC zilizopo mtaa wa Msimbazi,
Kariakoo jijini Dar es Salaam mchana huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
Simba, Damas Ndumbaro amesema kamati yake iliyokutana jijini Dar es Salaam
jana, imeamua uchaguzi huo ufanyike Juni 29 kupata Rais, Makamu wa Rais na
wajumbe wa kamati mpya ya utendaji ya Simba."Kamati
yangu ina watu makini, waadilifu na wenye mawazo chanya kwa klabu ya Simba.
Mara baada ya msajili kupitisha katiba juzi, jana tulikutana mara moja kupanga
ratiba ya uchaguzi. Hatutakuwa na huruma dhidi ya watu watakaokiuka kanuni za
uchaguzi," amesema Ndumbaro mwenye PhD ya Sheria.
Kuchelewa kwa
uchaguzi huo kunaufanya uongozi wa sasa chini ya mwenykiti Ismail Aden Rage
kuzidisha muda wake wa miaka nminne tangu Mei 10, 2010 unaolizika Mei 10 mwaka
huu, Jumamosi ijayo.
RATIBA YA MCHAKATO UCHAGUZI SIMBA SC
Mei 9, 2014: Kuanza kutoa fomu
Mei 14, 2014: Kurudisha fomu
Mei 17, 2014: Uhakiki wa fomu za wagombea
Mei 19, 2014: Kutangaza majina ya wagombea
Mei 20, 2014: Kupokea pingamizi dhidi ya wagombea
Mei 25, 2014: Kusikiliza pingamizi
Mei 27, 2014: Usaili wa wagombea
Mei 29, 2014: Kutangaza matokeo ya usaili
Mei 30, 2014: Masuala ya kimaadili
Juni 2-9, 2014: Kukata rufaa kamati ya rufaa
Juni 2-7, 2014: Maamuzi ya kamati ya maadili
Juni 10-12, 2014: Kusikiliza rufaa Juni 8-12
Juni 16, 2014: Kukata rufaa kamati ya rufaa ya maadili
Juni 16-20, 2014: Maamuzi ya mwisho ya kamati ya rufaa na kamati ya rufaa ya maadili
Juni 21-23, 2014: Kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
Juni 24-28, 2014: Kampeni
Juni 29, 2014: Uchaguzi mkuu

Chanzo:Binzubeiry
0 comments:
Post a Comment