Wakongo kuchezesha Tanzania na Nigeria.
Shirikisho la Soka la Afrika-CAF limeteua waamuzi
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC kuchezesha mchezo kati ya timu ya
taifa ya Tanzania-Ngorongoro Heroes na Nigeria.
Taarifa ta TFF imeeleza kuwa Mchezo huo wa mchujo kusaka tiketi ya kucheza
fainali za 19 za vijana chini ya umri wa miaka 20 zinazotarajiwa kufanyika
nchini Senegal mwakani, utachezwa mwishoni mwa wiki hii katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Waamuzi hao wataongozwa na Jean-Jacques Ndala Ngambo
atakayesaidiwa na Oliver Safari Kabene, Nabina Blaise Sebutu na Mupemba Ignace
Nkongolo. Kamishna wa mechi hiyo namba 37 ni Poiret Antoine Ralph Danny kutoka
Shelisheli.
0 comments:
Post a Comment