Friday, 16 May 2014

Zimbabwe kuwasili kesho



Timu ya Zimbabwe (Mighty Warriors) inawasili kesho alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 27. Kesho saa 4 asubuhi (Mei 17 mwaka huu) Kocha wa timu hiyo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zinaanza kuuzwa kesho (Mei 17 mwaka huu) kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, OilCom Ubungo, Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala. Viingilio ni sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 tu.
Katika hatua nyingine, mdau mmoja wa mpira wa miguu ambaye hataki jina lake litajwe ameahidi kutoa Sh. Milioni 5 kwa wachezaji wa Taifa Stars iwapo wataifunga Zimbabwe.
TFF inamshukuru mdau huyo, na linatoa mwito kwa wadau wengine wajitokeze kutoa motisha kwa Taifa Stars. Bonasi ya TFF kwa wachezaji wa Taifa Stars itatolewa kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

0 comments:

Post a Comment