Baada ya kupata ulaji Uarabuni,Mkwasa apongezwa na TFF.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limempongeza Kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa kwa kupata ajira ya ukocha msaidizi katika klabu Shoalah nchini Saudi Arabia.TFF inatoa mwito kwa makocha wengine kuiga mfano wa Mkwasa, kwani kufundisha mpira wa miguu nje ya Tanzania si tu kunawaongezea ujuzi bali pia kunawapa fursa ya kufanya kazi katika mazingira tofauti
Huko nyuma baadhi ya makocha wa Tanzania kama Mansour Magram, Kinanda Zakaria na Sunday Kayuni waliwahi kufundisha mpira wa miguu nje. Tangu wakati huo hakuna rekodi zinazoonesha kuwa kina makocha wazawa wanaofundisha nje
0 comments:
Post a Comment