Tuesday, 24 June 2014

Manchester United yakaribia kumnasa Herrera.

Manchester United wanakaribia kumsaini Kiungo wa Athletic Bilbao, Ander Herrera, kwa Dau la Pauni Milioni 30.
Msimu uliopita, katika Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho, Man United walishindwa kumsaini Kiungo huyo mwenye Miaka 24.
Dili hii inatarajiwa kukamilika baadae hii Leo na Herrera atakuwa Mchezaji wa kwanza kununuliwa na kocha mpya wa Man United, Louis van Gaal, ambae hivi sasa yuko Brazil akiiongoza Timu ya Taifa ya Uholanzi ambayo itacheza na Mexico kwenye hatua ya mtoano Fainali za Kombe la Dunia.
Kununuliwa kwa Herrera, ambaye ndiye alikuwa Kiungo nguzo ya Atletico Madrid iliyotwaa Ubingwa wa La Liga huko Hispania, kutaimarisha idara ya Kiungo ya Man United iliyodhoofika kwa kustaafu Paul Scholes na, ukimwondoa Marouane Fellaini aliyesainiwa Msimu uliopita, haijanunua Kiungo yeyote kwa Miaka 6 sasa.
Ingawa yuko huko Brazil, Van Gaal, ambae ataanza kazi yake rasmi Old Trafford baada kumalizika kwa Fainali za Kombe la Dunia, ameshaanza kujenga Kikosi kwa kuwaongezea Mikataba Antonio Valencia ns Patrice Evra.

0 comments:

Post a Comment