Thursday, 26 June 2014

Hatua ya mtoano Nigeria na Ufaransa,Ghana kujaribu bahati yao leo

Ufaransa na Ecuador walitoka suluhu katika Mechi ya mwisho ya Kundi E la Fainali za Kombe la Dunia na Ufaransa kusonga mbele wakiwa Washindi wa Kundi huku Ecuador wakitupwa nje baada ya Switzerland kuifunga Honduras mabao 3-0 kwenye Mechi nyingine ya Kundi hili.

Ecuador walimaliza Mechi  wakiwa wachezaji  10 baada ya Mchezaji wa Manchester United Antonio Valencia, ambae ni Nahodha wa Ecuador, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Kipindi cha Pili kwa rafu mbaya kwa Lucas Digne.
Katika mchezo mwingine mabao matatu ya Mchezaji wa Bayern Munich Xherdan Shaqiri imewapa Switzerland ushindi wamabao 3-0 dhidi ya Honduras na kufuzu kutoka Kundi E na kuipiku Ecuador.
Switzerland sasa watacheza na Argentina kwenye Raundi ya Pili ya Mtoano.
Honduras wamemaliza Mechi zao za Kundi E wakiwa mkiani baada ya kufungwa Mechi zao zote 3.
Mapema jana Argentina iliwafunga Nigeria 3-2 lakini timu zote zimefuzu hatua ya mtoano baada ya Iran kupigwa mabao 3-1 na Bosnia ambapo Nigeria ilikuwa na alama 4 ilhali Argentina wakimaliza na alama zao 9.
Baada ya michezo hiyo leo ratiba ni kama ifuatavyo
ALHAMISI, JUNI 26, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
United States v Germany
G
Arena Pernambuco
1900
Ureno v Ghana
G
Nacional
2300
Korea kask v Belgium
H
Arena Corinthians
2300
Algeria v Urussi
H
Arena da Baixada
Timu ambazo zimeingia hatua ya mtoano ratiba yao ni kama ifuatavyo
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil v Chile
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia v Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54



JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo


0 comments:

Post a Comment