Chile yafungashwa virago na Brazil
Brazil wameitoa Chile katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia katika Uwanja wa Belo Horizonte, kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.Julio Cesar alikuwa shujaa baada ya kuokoa penalti mbili za Alexis Sanchez na Mauricio Pinilla wakati Gonzalo Jara aligongesha mwamba, huku Marcelo Diaz na Charles Aranguiz wakifunga.
Brazil walitangulia kufunga kwa Bao la
Dakika ya 18 la David Luiz alieunganisha Mpira uliopigwa Kona na Neymar
na kugongwa na Thiago Silva.
Chile walisawazisha kwenye Dakika ya 32 kwa Bao la Alexis Sanchez.
Kipindi cha Pili Hulk aliifungia Brazil
Bao la Pili lakini Msaidizi wa Refa Howard Webb kutoka England
aliashiria Mbrazil huyo alishika kabla kufunga.
Hadi Dakika 90 kumalizika mabao yalikuwa
1-1 na Nyongeza ya Dakika 30 haikuzaa Mshindi na Mechi kuingia Mikwaju ya Penati ambazo Brazil walishinda kwa Penati hizo 3-2 na kutinga
Robo Fainali ambapo watakutana na Mshindi kati ya Colombia na Uruguay
wanaocheza baadae Leo.

0 comments:
Post a Comment