Saturday, 28 June 2014

Kesho bingwa wa mieleka kupatikana katika money in the bank.

Hatimaye kesho (Juni 29)wanaume 8 watakuwa ulingoni kupambana katika mchezo wa  WWE Money in the Bank ambapo wanamieleka Roman Reigns, John Cena, Randy Orton, Bray Wyatt, Bingwa wa Marekani  Sheamus, Cesaro na  Alberto Del Rio watashindana katika mchezo unaohusisha ngazi ili kumpata bingwa mpya wa uzito wa juu duniani.
Hapo kabla bingwa anayemiliki mkanda huo Daniel Bryan amejitoa rasmia  June 9 baada ya  kutopona vema na bado hajakamilisha matibabu yake.
Kwenye historia  John Cena, Del Rio, Kane,Sheamus na Orton wamewahi kuchukua ubingwa huo wa dunia lakini  Reigns, Wyatt na  Cesaro hawajawahi kubeba ubingwa huo.
Money in the bank ni mchezo ambao wanamieleka hupigana na kisanduku  kufungwa  juu na kuning'inia na atakayeshinda ataweka ngazi ili atoe mkanda huo na ndipo atakuwa mshindi .
Kwa matokeo na nini kinaendelea usikose kufuatilia mtandao huu Sports4lifetz

0 comments:

Post a Comment