Sunday, 15 June 2014

Colombia,Costa Rica mambo safi kombe la dunia

Mabao ya Dakika ya 5 la Pablo Armero, Dakika ya 58 Teofilo Gutierrez na Dakika ya 91 la James Rodriguez  yamewapa ushindi wa mabao 3-0 Colombia walipocheza na Ugiriki kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi C la Fainali za Kombe la Dunia Jijini Belo Horizonte Nchini Brazil.
Ktaika mchezo mwingine Costa Rica imeanza vema Kombe la dunia baada ya kuichapwa mabao 3-1 Uruguay katika mchezo wa Kundi D Fortaleza, Brazil.
Uruguay ilitangulia kupata bao la penalti la Edinson Cavani dakika ya 24 kabla ya kinda wa Arsenal, Joe Campbell kuisawazishia Costa Rica dakika ya 54.
Huku mshambuliaji nyota wa Uruguay, Luis Suarez ambaye ni majeruhi akiwa benchi, alishuhudia jahazi la timu yake likizama kwa mabao mawili zaidi kipindi cha pili.
Oscar  Duarte aliifungia Costa Rica bao dakika ya 57 kabla ya Marcos Urena kufunga la tatu dakika ya 84.
Katika mpambano huo Maxi Parera alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90  kwa kumchezea rafu Campbell.

0 comments:

Post a Comment