Sunday, 15 June 2014

Waamuzi wa mechi za leo na kesho jumatatu,Mserbia miaka 41 kuchezesha Ureno na Ujerumani

Shirikisho la soka duniani FIFA imetangaza waamuzi watakaochezesha Mechi zijazo za Fainali za Kombe la Dunia za Jumatatu.
Mwamuzi kutoka Ecuador, Carlos Vera, akiwa amebakisha Siku 9 kutimiza Miaka 38, atasimamia Mechi kati ya Iran na Nigeria.
Vera ni mwamuzi wa Kimataifa tangu 2007 na ameshachezesha Mechi kubwa ikiwa pamoja za Copa America 2011, Copa Libertadores 2008 na Kombe la Dunia kwa Klabu Mwaka 2012.
Mechi ya Ujerumani  v Ureno itakuwa chini ya mwamuzi Milorad Mazic kutoka Serbia mwenye Umri wa Miaka 41.
Ghana v USA itasimamiwa na mwamuzi  wa Sweden Jonas Eriksson, Miaka 40, ambae amewahi kuchezesha UEFA EURO 2012 na pia Mechi ya Mchujo ya Marudiano ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Jordan hapo Novemba 2013.
Waamuzi wa JUMAPILI Juni 15
-Switzerland v Ecuador [Mwamuzi: Ravshan IRMATOV toka Uzbekistan]
-France v Honduras [mwamuzia: Sandro RICCI toka Brazil]
-Argentina v Bosnia [Mwamuzi: Joel AGUILAR toka El Salvador]
Waamuzi wa  MECHI ZA JumatatuI Juni 16
-Germany v Portugal [Refa: Milorad Mazic toka Serbia]
-Iran v Nigeria [Refa: Carlos Vera toka Ecuador]
-Ghana v United States [Refa: Jonas Eriksson toka Sweden]

0 comments:

Post a Comment