Saturday, 14 June 2014

FIFA imemtetea mwamuzi wa Japan aliyechezesha Brazil na Croatia

Yuichi Nishimura
Shirikisho la soka duniani FIFA Limezungumzia utata uliotokea siku ya Alhamisi na pia imemtetea mwamuzi wa Japan Yuichi Nishimura baada ya kuipa  pelnati ya utata timu ya   Brazil katika mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya  Croatia.
Kocha wa Croatia alilalamika bada ya  uamuzi uliotolewa na mwamuzi Nishimura na kutoa pelnati baada ya mlinzi  Dejan Lovren kumuangusha mshambuliaji Fred.
Vyombop vy habari nchini Croatian wamelalamikia tukio hilo na kudai kuwa mwamuzi alifanya makosa. Lakini magazeti ya Brazil yameandika "arigato" –kwa maana ya ahsante mjapan .

Fifa imemtetea  Nishimura, lakii imesema kuwa hakuna maamuzi yaliyochukuliwa kama atachezesha mchezo mwingine.
Kiongozi wa waamuzi wa Fifa  Massimo Busacca amesisitiza kuwa  Nishimura amefuzu kuchezesha komb la duia.
Nishimura mwenye miaka , 42, amechaguliwa kuwa kocha bora mara mbili nchini   Japan katika  J-League .

0 comments:

Post a Comment