David Villa atua rasmi katika ligi ya MLS
Klabu ya New York City FC imethibitisha rasmi kuwa Mhispania ambaye anaongoza kwa kuifungia timu ya taifa mabao mengi David Villa amekuwa mchezaji wao wa kwanza Kusajiliwa katika ligi ya Marekani MLS.Mshambuliaji huyo wa zamani wa Valencia na Barcelona anaondoka Atletico Madrid baada ya kutumikia msimu moja na kufunga mabao 13 na kuisaidi klabu yake kufika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya tokea mwaka 1996.
“Siku zote katika kipaji changu najaribu kitu kipya na hii inaonesha kitu muhimu kwangu ”, Villa mwenye miaka 32 aliliambia mtandao wa New York City.
“Ninataka kuisaidia MLS iendelea kukua kwa kucheza,kufunga mabao na pia kuifanya New York City FC iwe klabu bora katika ligi hii.'alisema Villa
Villa ameichezea Hispania michezo 94 , amefunga mabao 56 na ametajwa katika kikosi cha wachezaji 23 kwenda katika kombe la dunia nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment