Tuesday, 3 June 2014

Fainali ya CECAFA Nile Basin kupigwa kesho huko Sudan

Hatimaye Fainali ya michuano  ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki (CECAFA) Nile Basin  itapigwa kesho ambapo AFC Leopards ya Kenya itamenyana na Victoria University ya Uganda katika Uwanja wa Khartoum, Sudan.
Hiyo inafuatia timu hiyo ya Uganda kuwatoa wenyeji, Al Shandy kwa bao 1-0 katika Nusu Fainali ya pili jana Uwanja wa Khartoum, baada ya Leopards kuing’oa Academie Tchite kwa mabao 2-0.

Bingwa wa michuano hiyo, ataondoka na kitita cha dola za Kimarekani 30, 000 (Sh. Sh. Milioni 50 za Tanzania) na mshindi wa pili atabeba dola 20, 000 (Sh. Milioni 33).
Mshindi wa tatu atakayepatikana katika mchezo baina ya Tchite na Shandy, ataondoka na dola 10 000 (Sh. Milioni 16.5).

0 comments:

Post a Comment