Falcao atupwa nje kikosi cha Colombia
Mshambuliaji Radamel Falcao wa klabu ya Monaco ya Ufaransa na timu ya taifa ya Colombia ameachwa kwenye Kikosi cha Wachezaji 23 kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia.
Falcao ndyie alikuwa Mfungaji Bora wa Colombia akiwa na mabao 9 kwenye
Mechi za Kundi la Amerika ya Kusini kwa ajili ya kufuzu Fainali za
Kombe la Dunia walipomaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Argentina na yeye
kuwa nyuma tu ya Wafungaji Bora wa Kundi hilo, Luis Suarez na Lionel
Messi.
Ingawa Falcao alikuwemo kwenye Kikosi
cha Awali cha Wachezaji 30 ikiwa ni mara ya kwanza kwake kurudi Uwanjani
tangu Januari alipofanyiwa upasuaji ya Goti, alishindwa kuonyesha
kama yuko fiti na atakuwa tayari kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Kombe la dunia inaanza Juni 12 na kumalizika Julai 13 ambapo Colombia wapo KUNDI C pamoja na Ugiriki, Ivory Coast na Japan.
COLOMBIA-Kikosi kamili:
Makipa: David Ospina (Nice), Faryd Mondragon (Deportivo Cali), Camilo Vargas (Independiente Santa Fe).
Mabeki: Camilo Zuniga (Napoli), Pablo Armero (West Ham), Cristian Zapata (Milan), Mario Yepes (Atalanta), Carlos Valdes (San Lorenzo), Santiago Arias (PSV), Eder Alvarez Balanta (River Plate).
Viungo: James Rodriguez
(Monaco), Abel Aguilar (Toulouse), Carlos Sanchez (Elche), Fredy Guarin
(Inter Milan), Juan Fernando Quintero (Porto), Aldo Ramirez (Morelia),
Alex Mejia (Atleico Nacional), Victor Ibarbo (Cagliari), Juan Guillermo
Cuadrado (Fiorentina).
Washambuliaji: Jackson Martinez (Porto), Teofilo Gutierrez (River Plate), Carlos Bacca (Sevilla), Adrian Ramos (Borussia Dortmund).
0 comments:
Post a Comment