Thursday, 26 June 2014

Fernando ndani ya Manchester City.

Klabu ya Manchester City  imemsajili kiungo wa  Porto  Fernando Francisco Reges  kwa uhamisho wa  €15 million (£12m), mabingwa hao wa EPL wamethibitisha rasmi.
City walikuwa wanahitaji huduma ya  Fernando na Eliaquim Mangala baada ya mwezi januari kushindikana lakini safari hii wamefanikiwa kwa Fernando ila Mangala kuna taarifa kwamba amesaini kuendelea kuitumikia klabu yake ya Porto.
City imeeleza kuwa uhamisho wa mchezaji huyo unakuwa mgumu kidogo kwa sasa baada ya wakala wa Fernando, Antonio Araujo, kudai kuwa uhamisho huo ufanyike mwezi ujao.

0 comments:

Post a Comment