Thursday, 26 June 2014

Messi,Neymar au RVP,Muller kubeba kiatu cha dhahabu?

Messi na Neymar
Huko Brazil michezo ya makundi yatamalizika hii leo huku mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora Zikianza kuchukua nafasi.
Inavyoonekana kwa sasa Messi na  Neymar wameanza kuzungumzwa kuwa mmojawao atabeba kiatu hicho. Messi alifunga mabao mawili wakati Nigeria wakilazwa  3-2 na Argentina wakati Neymar alifunga amabao mawili wakati Brazil ikiiangamiza Cameroon 4-1.
RVP
Messi, aliyefikisha miaka  27 juzi jumanne, anakuwa mchezaji wa tatu wa Argentina kufunga mabao katika michezo mitatu mfululizo baada ya  Gabriel Batistuta na Oreste Corbatta na kuisaidi timu yake kuingia 16 bora
Neymar naye amefikisha mabao manne ila hakufunga bao Brazil ikicheza na Mexico,kuna baadhi ya wachezaji wakiendelea kufumania nyavu inawezekana Neymar na Messi wakaenguliwa.
Shaqiri











Wachezaji ambao wana mabao 3 kila moja ni

Thomas Muller (Ujerumani ), Robin Van Persie, Robben (Uholanzi), Karim Benzema (Ufaransa) pamoja na E Valencia (wa Ecuador),Rodriguez (Colombia), Shaqiri (Switzerland).
Wachezaji wenye mabao mawili ni pamoja na  2 – Cahill (Australia), Mandzukic (Croatia), Suarez (Uruguay), Gervinho (Ivory Coast), Depay (Holland), Perisic (Croatia), Martinez (Colombia), Dempsey (USA), Bony (Ivory Coast), A Ayew (Ghana), Musa (Nigeria).

0 comments:

Post a Comment