Saturday, 14 June 2014

Franz Beckenbauer asimamishwa siku 90

Nguli wa Ujerumani Franz Beckenbauer  amefungiwa kutojihusisha na masuala ya mchezo wa mpira wa migu, kwa muda wa siku 90, hii ni kutokana kwake kukataa kushirikiana na uchunguzi wa kuteuliwa Qatar  kama mwenyeji wa kombe la dunia 2022.
Mwanasheria Michael Garcia ndie alieomba kifungo hicho, baada ya kuripoti kuukosa ushirikiano kutoka kwa nguli huyo kutoka Ujerumani ambae ameshinda na timu ya Taifa ya nchi yake kama Mchezaji na pia kama Mwalimu.
Katika moja ya utetezi wake kuhusu maswali aliyoletewa kuhusu uchunguzi, anasema alihitaji Maswali yaandikwe kwa lugha yake, Kijerumani, kwakuwa Michael Garcia alitumia kiingereza kigumu kwake kuelewa.
Lakini hilo likaonekana kama ni njama za Franz kukwepa uchunguzi huo.
Franz Beckenbauer alikuwa katika kamati ambayo ilipiga kura kuchagua Qatar kama mwenyeji 2022, huku akisisitiza hatasema nchi gani aliyoipigia kura, na haina uhusiano na kupewa chochote kuhusu kura yake.
Uchunguz unaendelea kuangalia nini kilifanyika katika upigwaji kura wa kuchagua mwenyeji wa michuano pendwa duniani, ikisemekana Qatar  ilitoa hongo kupata uenyeji huo. Ikichukuliwa kwamba Qatar ni nchi ya jangwa yenye joto kali, sehemu ambayo kandanda ni ngumu sana kuchezeka.

0 comments:

Post a Comment