FIFA yamwaga tiketi zingine sokoni kwa ajili ya kombe la dunia
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linatarajia kuweka sokoni tiketi za mwisho zipatazo 180,000 kwa ajili ya mashabiki kesho.Tiketi kwa ajili ya mechi zote 64 bado zinapatikana na zinaweza kununuliwa kupitai mtandao pamoja na vituo vya tiketi vilivyowekwa katika viwanja 12 vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo nchini Brazil.
Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa tiketi hizo zinatarajiwa kuwekwa sokoni ifikapo usiku wa manane ambapo zitaungana na tiketi zingine ambazo bado ziko sokoni.
Mechi ya kwanza ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa Juni 12 jijini Sao Paulo wakati wenyeji Brazil watakapoikaribisha Croatia.
0 comments:
Post a Comment