Taifa Stars kuingia kambini Juni 11,soma nani na nani kucheza na makundi pia.
Timu ya taifa ya soka Tanzania Taifa Stars, chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij, inatarajia kuingia kambini Jumatano ijayo Juni 11 2014 kwa ajili ya kujiwinda na mchezo dhidi ya Msumbiji kuwania kupangwa hatua ya makundi ili kusaka tiketi ya fainali za AFCON zitakazochezwa Morocco hapo mwakani.
Taifa Stars imewasili kutokea Harare ambako ilifanikiwa kufuzu hatua inayofuata baada ya kuiondoa Zimbabwe kwa jumla ya magoli 3 – 2.
Stars ilishinda bao 1-0 katika
mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam na kufanikiwa kutoka sare ya 2-2
mjini Harare, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Boniface Wambura amesema timu hiyo inataraji kuingia kambini kwa mara nyingine
kujiwinda dhidi ya Msumbiji Jumatano ijayo kwasababu mwalimu anatakiwa
kupata muda wa kutosha kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza mechi
zilizopita.
Taifa Stars inataraji kucheza dhidi ya Msumbiji hapo Julai 19 au 20 mwaka huu pamoja na timu nyingine za ukanda wa CECAFA Kenya, Uganda na Rwanda ambazo zimepenya hatua inayofuata.
Iwapo Stars itafuzu itapangwa kundi la F,soma zaidi makundi na nchi zilizoingia hatua ya pili.
Ratiba
Tanzania v Mozambique
Lesotho v Kenya
Uganda v Equatorial Guinea
Congo Brazzaville v Rwanda
Botswana v Guinea-Bissau
Sierra Leone v Seychelles
Benin v Malawi
Lesotho v Kenya
Uganda v Equatorial Guinea
Congo Brazzaville v Rwanda
Botswana v Guinea-Bissau
Sierra Leone v Seychelles
Benin v Malawi
AFCON 2015 MAKUNDI:
Group A : Nigeria, South Africa, Sudan, Congo/Rwanda
Group B : Mali, Algeria, Ethiopia, Benin/Malawi
Group C : Burkina Faso, Angola, Gabon, winner Lesotho/Kenya
Group D : Ivory Coast, Cameroon, DR Congo, Sierra/Seychelles
Group E : Ghana, Togo, Guinea, Uganda/Equatorial Guinea
Group F : Zambia, Cape Verde, Niger, Tanzania/Mozambique
Group G : Tunisia, Egypt, Senegal, Botswana/Guinea Bissau

0 comments:
Post a Comment