Miaka 14 bila kubeba kombe la dunia,ila bado ni beki bora zaidi duniani.
Paolo Cesare Maldini Alizaliwa tarehe 26 June 1968,ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Italia,anacheza beki ya upande wa kushoto au kati.Katika kipaji chake Misimu yote 24 aliitumikia klabu ya AC Milan, kabla ya kustaafu soka akiwa na miaka 41 mwaka 2009, Kwa sasa anatajwa kama mtu anayeheshimika ndani ya klabu na pia ni mchezaji mwenye mafanikio akiwa na AC Milan
Leo ni siku yake ya kuzaliwa.Alishinda ligi ya mabingwa barani Ulaya mara 5,hali kadhalika amebeba ubingwa mara 7 wa Serie A ,amebeba Coppa Italia mara 1, Supercoppa Italiana mara 5, European Super Cups ambeba mara 5,
Ameichezea Italia kwa miaka 14 , alianza kucheza timu ya Italia mwaka 1988 kabla ya kustaafu soka la kimataifa mwaka 2002 akicheza michezo 126.
Ameshiriki kombe la dunia mara 4 ingawa hajawahi kubeba taji la kombe la dunia akiwa na timu ya Italia , alifika fainali katika kombe la dunia mwaka 1994 na Euro 2000, pia alifika nusu fainali kombe a dunia mwaka 1990 na Euro 1988.
Maldini bado ataheshimika kama beki mzuri duniani.Alishinda tuzo ya beki bora kwenye tuzo ya UEFA Club Football akiwa na miaka 39. Beki pekee aliyepewa tuzo kabla ya Fabio Cannavaro mwaka 2006. Alichaguliwa kuwa beki katika ile timu bora ya dunia yaani FIFA World Cup Dream Team,na mwaka 2004 alitajwa kwenye list ya wachezaji 125 wa soka katika sherehe ya miaka 100 ya FIFA.
0 comments:
Post a Comment