Homa ya Dengue yaanza kutisha kombe la dunia,akina Ronaldo na Mikel Obi mhhhh
Zikiwa zimebaki siku 11 kabla ya fainali za kombe la dunia,Mji wa Brazil ambao utafikiwa na nyota wa kireno Cristiano Avveiro dos Santos Ronaldo na nyota wa Nigeria John Mikel Obi kwa ajili ya mazoezi ya kombe la dunia uko hatarini kukumbwa na ugonjwa hatari wa dengue .Wafanyakazi wanajitahidi kuwamaliza kabisa mbu wanaoambukiza ugonjwa huo kabla ya timu za Ureno na Nigeria kutua.
Watu 32 384 wameambukizwa ugonjwa wa dengue mwaka huu kusini mashariki mwa mji wa Sao Paulo. Watu watatu wamefariki dunia.
"Ni rekodi ya aina yake. ni zaidi ya ile ya mwaka 2007 ambapo watu 11 500 waliathirika ," alisema Andrea Von Zuben, anayehusika na utokomezaji wa dengue.
Dengue in ugonjwa uliosambaa duniani katika nchi za ukanda wa joto. Takribani asilimia 40 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi zenye ugonjwa huu. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani matukio milioni 5 ya Dengue yanatolewa taarifa kila mwaka. Watu laki 5 hulazwa hospitali kwa kuathirika na Dengue kali.
Dalili za ugonjwa huu ni homa, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu
Shirikika la afya duniani WHA limesema kuwa watu wanapaswa Kuangamiza mazalio ya mbu
kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au kunyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwivya mbu kwenye madimbwi hayo pia kufeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
Mapema mwezi mei kocha wa Ureno Paulo Bento alitembelea maeneo hayo na kuhakikishiwa kuwa kabla ya June 11 wadudu hao watatokomezwa moja kwa moja.
Jeshi nalo limeanza kusaidia ambapo tani 83 000 za takataka na nyumba zilizohatarini zimenyunyiziwa dawa.
Timu za Nigeria na Ureno zinatarajiwa kutumia mji huo wa Sao Paulo kwa ajili ya maandalizi ya kombe la dunia ambapo taji lipo mikononi mwa Hispania.
0 comments:
Post a Comment