Sunday, 1 June 2014

Mbeya City yatupwa nje mashindano ya Nile Basin

Klabu ya Mbeya City  imetolewa nje ya Mashindano ya  CECAFA NILE BASIN  kwa mwaka wa 2014  baada kufungwa na Victoria University 1-0 kwa kwa njia ya  Penati kwenye Mechi ya Robo Fainali huko Khartoum Stadium jumamosi hii.
Penati hiyo ilitolewa Dakika ya 74 na pia Mbeya City kumaliza ikiwa na wachezaji 10 baada ya Kibopile Hamad kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Victoria University ya Uganda watacheza na Mshindi wa Ahly Shandi Vs Malakia kwenye Nusu Fainali.

0 comments:

Post a Comment