Imekula kwa Manchester United,Muller ajifunga Munich Hadi 2019
![]() |
Muller na Lahm |
Nahodha Lahm kwa sasa atawatumikia mabingwa wa Bundesliga hadi June 2018, wakati Muller - ambaye alikuwa akitajwa kuondoka atabaki Allianz Arena hadi June 2019.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa klabu Karl-Heinz Rummenigge.
"Philipp Lahm na Thomas Muller ni watu muhimu sana ndani ya FC Bayern," Rummenigge alisema hayo kupitia mtandao wa klabu.
"Wamekuwa waaminifu kwa klabu yetu tokea waanze kucheza na bado tuna malengo ya baadaye na hawa vijana.
Lahm alijiunga na Bayern akiwa na umri wa miaka 11 na inawezekana akamaliza kipaji chake kwa kuitumikia Bayern .
Alipoulizwa kuhusu mkataba huo Lahm alieleza kuwa anafuraha zaidi kwa kuendelea kuitumikia klabu na kumaliza kipaji chake Alianz Arena
Muller alikuwa anazungumziwa sana kuwakacha Bavaria, ili ajiunge na Manchester United chini ya kocha wake wa zamani Louis van Gaal
Kwa maana hiyo sasa wachezaji ambao walitakiwa na Van Gaal akina Robben,Muller na Kroos wameota mbaya ndani ya Old Traford.
Muller mwenye miaka 24 amesema kuwa taarifa zote zilizosemwa kuhusu yeye sasa zimefika mwisho na yuko tayari kuitumikia klabu yake.
Lahm na Muller kwa sasa wapo Brazil kujiandaa na michezo ya kombe la dunia ambayo itaanza kesho na wana nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha Joachim Low.
0 comments:
Post a Comment