Tuesday, 10 June 2014

Luke Shaw aanza kunukia Old Traford,akitua tu atalipwa £160,000-kwa wiki.

Luke Shaw
Mchezaji Luke Shaw wa klabu ya Southampton amekubaliana na klabu ya  Manchester United na wataingia kwenye mjadala wa vipengele binafsi na atakuwa akilipwa mshahara wa  £160,000-kwa wiki,kwa mujibu wa mtandao wa  Goal.com.

Mlinzi huyo wa timu ya taifa ya Uingereza , ambaye atafikisha miaka  19   July 12, atakuwa mchezaji mdogo atakayelipwa zaidi duniani iwapo akikamilisha dili hilo la kwenda Old Trafford.
Chelsea wamejitoa katika mbio hizo baada ya mkataba wake kuwa mrefu ndani ya Southampton lakini Manchester United wamefanikisha hilo.

Kocha Jose Mourinho anamhusudu sana kijana huyo mwenye miaka  18 na hii inakuja baada ya beki wa kushoto  Ashley Cole kutoongezewa mkataba ndani ya vijana hao wa Mourinho.
United walitoa kiasi cha £27 mil kwa ajili ya  Shaw baada ya msimu wa ligi kumalizika lakini ofa hiyo ilikataliwa.
Kwa mujibu wa Southampton haitawaruhusu   Shaw,  ama Adam Lallana na wachezaji wengine mpaka pale kocha mpya atakapopatikana.
Lakini, Shaw baada ya ligi kumalizika alionekana kuonesha nia ya wazi ya kwenda  Old Trafford na United imemweka katika wachezaji muhimu watakaosajiliwa msimu huu.

Iwapo atatua Old Traford atakuwa anapambana na Patrice Evra  katika utawala wa  Louis van Gaal.
Shaw kwa sasa anajiandaa na kombe la dunia akiwa na timu yake lakini atakuwa akianzia benchi kutokana na vita ya namba mbele ya Leighton Baines kwa upande wa beki ya kushoto.

0 comments:

Post a Comment