Inter Milan yamteua Zanetti kuwa makamu wa rais,jezi namba 4 stop
Klabu ya Inter Milan imeamua kusimamisha matumizi ya
jezi yenye namba nne mgongoni kwa heshima ya Javier Zanetti na wanatarajia
kumteua beki huyo wa kulia aliyestaafu hivi karibu kuwa makamu wa rais wa klabu
hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mkongwe huyo wa Argentina aliamua kutundika daruga
zake rasmi mwaka huu baada ya kuitumikia Inter kwa kipindi cha miaka 19, ambapo
alifanikiwa kushinda mataji matano ya Serie A, manne ya Kombe la Italia, taji
la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia.
Rais wa klabu hiyo Erick Thohir amebainisha kuwa
sasa Inter itaondoa namba aliyokuwa akivaa nyota huyo kwenye jezi zake ili
kumpa heshima kwa kipindi alichofanya kazi hapo pamoja na kumpa nafasi hiyo
muhimu kwenye timu hiyo.
Thohir amesema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha
bodi walichokutana kujadili jinsi ya kumuenzi mkongwe huyo kwa utumishi wake
uliotukuka katika timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment