Tuesday, 1 July 2014

Timu za Afrika sasa wajiandae kwa ajili ya kombe la dunia 2018

Timu zote za Afrika zimeaga mashindano ya kombe la dunia baada ya Ujerumani kuiondoa Ageria mchezo uliopigwa  Mjini Porto Alegre Nchini Brazil na kuhitaji Dakika 120 ili Ujerumani kushinda mabao 2-1.
Hiyo inakuja baada ya  Nigeria kufungwa 2-0 na Ufaransa na kutolewa nje ya Mashindano haya.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, Timu nyingine za Afrika zilizoshiriki na kutupwa nje Hatua ya Makundi ni Ghana, Cameroon na Ivory Coast.
Hadi Dakika 90 matokeo yalikuwa 0-0.
Lakini ndani ya Kipindi cha Kwanza cha Dakika za Nyongeza 30, Dakika 2 tu tangu kianze, Andre Schurrle akaifungia Bao Ujerumani  na Mesut Ozil kuongeza la Pili Dakika ya 119 na kuwafanya waongoze 2-0.
Algeria walipata Bao lao moja mwishoni, Dakika ya 120, kupitia, Abdelmoumene Djabou.
Kwa manatiki hiyo sasa timu zote za Afrika zijiandae kwa ajili ya fainali zijazo kule nchini Urusi 2018.
Ratiba ya leo
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 55 Argentina v Switzerland Corinthians Sao Paulo
2300 56 Belgium v USA Fonte Nova Salvador






ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Ufaransa  v Ujerumani [57] ROBO FAINALI Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro
2300 Brazil v Colombia [58] ROBO FAINALI Estadio Castelão, Fortaleza
JUMAMOSI, JULAI 5, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Argentina/Switzerland v Belgium/USA [59] ROBO FAINALI Nacional, Brasilia
2300 Netherlands v Costa Rica [60] ROBO FAINALI Arena Fonte Nova, Savador
NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Mshindi 57 v Mshindi 58 [61] NUSU FAINALI Estadio Mineirão, Belo Horizonte
JUMATANO, JULAI 9, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Mshindi 59 Mshindi 60 [62] NUSU FAINALI Arena Corinthians, Sao Paulo
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62 MSHINDI WA 3 Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2200 Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62 FAINALI Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

0 comments:

Post a Comment