John Cena aibuka kidedea,akina Batista hoi mbele ya Shield
Usiku wa jumapili yaani jana kule nchini Marekani wanamieleka mbalimbali walipanda ulingoni katika mchezo wa PAYBACK .Mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na wapenda mieleka ni ule wa kikundi cha Shield na Evolution pamoja na mchezo baina ya John Cena dhidi ya Bray Wyatt.
Kwa mara nyingine tena kikundi cha shield kimeendelea kuwa tishio baada ya kuwagaragaza akina Randy Orton,Batista na Triple H ambao wanaunda kikundi cha Evolution.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Shield kushinda mbele ya Evolution kwani katika mchezo uliopigwa mapema wiki iliyopita walishinda katika mchezo wa Extreme Rules.
John Cena alionesha jinsi gani alivyokuwa na uwezo baada ya kumpiga Bray Wyatt kwenye mchezo ulioitwa Last Man Standing .
Sheamus ambaye ni bingwa wa Marekani alimpiga Cesaro na kutwaa ubingwa wa United States .
Bad News Barrett alibeba ubingwa wa mabara baada ya kumpiga bingwa wa zamani wa uzito wa juu Rob Van Dam.
Ryback na Curtis Axel walishinda dhidi ya Cody Rhodes na Goldust
Rusev alimpiga Big E.
Kwa mara nyingine ubingwa wa akina dada maarufu kama Divas umebebwa tena na Paige baada ya kumpiga Alicia Fox.
El Torito alishinda mbele ya Hornswoggle
0 comments:
Post a Comment