U15 Tanzania kutua leo wakitokea Botswana.
Timu ya Tanzania ya wachezaji
wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili katika Michezo ya
Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana inawasili leo
(Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
U15 ambayo imeshinda mechi tatu,
sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways
ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania ambayo imepata medali za
fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini ya Kocha Abel Mtweve
ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka
sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo
walioibuka mabingwa.
Wachezaji 16 waliounda kikosi cha
Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede
Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga,
Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro
Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
0 comments:
Post a Comment