Friday, 20 June 2014

Kaka amfuata David Villa kule Marekani.

Kiungo wa klabu ya AC Milan  Ricardo Izecson dos Santos Leite  maarufu Kaka amefikia mahali pazuri katika maongezi na klabu  ya Orlando City ambapo atajiunga hapo  January 2015, katika ligi ya Marekani, MLS imeeleza taarifa ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye miaka  32 alijiunga tena na klabu ya Milan baada ya kuitumikia klabu ya Real Madrid miaka minne pasipo mafanikio.
Kaka  ambaye mapema  alizungumza na klabu hiyo kwa sasa mambo yanakaribia kumalizika.

“Klabu ya  Orlando City imefikia hatua ya mwisho na  Kaka. kwa sasa tumefika makubaliano binafsi,
 Kaka  atajiunga na Orlando City SC hapo January 2015  kabla ya kuanza kwa  MLS." taarifa ya klabu ya Orlando City.

Mbrazil huyo amaefunga mabao 29  katika michezo 87 kwa upande wa  selecao ameshinda taji la ligi ya mabingwa ulaya akiwa na Milan mwaka 2007 na ameshinda taji la  Serie A na La liga akiwa na Madrid.
Kaka siku za hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa angependelea zaidui kucheza Marekani iwapo ataondoka Milan.
Iwapo Kaka  atafanikiwa kujiunga na Orlando City,  atakuwa mchezaji wa pili mwenye jina kubwa duniani kujiunga na ligi ya MLS kufuatia  David Villa kujiunga na New York akitokea Athletico Madrid.

0 comments:

Post a Comment