Tiki-taka imekwisha kwa upande wetu-Hispania
![]() |
Cassilas na Iniesta baada ya kufungwa na Chile. |
Kipigo cha mabao 2-0 walichopata kutoka kwa Chile jana na kile cha mabao 5-1 kutoka kwa Uholanzi kinamaanisha kwamba mabingwa hao wa michuano ya Ulaya mwaka 2012 hawataweza kufuzu katika hatua inayofuata kutoka katika kundi B.
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Alonso mwenye umri wa miaka 32 amesema walikuwa hawana uchu au morali iliyohitajika kwa ajili ya kushinda michuano hiyo.
Hispania ni maarufu kucheza soka ya kutumia pasi fupi ya kuwatumia sana viungo marufu kama tiki-taka.
Alonso aliongeza kuwa furaha na mafanikio waliowahi kupata anadhani muda wake umefikia kikomo na anafikiri wakati umefika wa kufanya mabadiliko.
Naye Kocha wa Hispania Vicente Del Bosque amesema kuna gharama ya kikosi chake kutolewa na kudokeza kuwa uongozi wake wa miaka sita wa timu hiyo unaweza kuwa umefikia kikomo.
Kocha huyo alindelea kudai kuwa kwasasa watakuwa na muda wa kuchambua na pia kutakuwa na muda wa kufikiri kama kuna mabadiliko yoyote yatahitajika kufanyika ili waweze kutoa uamuzi utakaokuwa na tija kwa soka la Hispania.
0 comments:
Post a Comment