Kesi ya Wambura kumalizwa leo,jana ilishindikana
![]() |
| Michael Wambura |
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amesema kuwa jana walifanya kikao hadi Saa 4:30 usiku bila kumaliza na wamepanga kukutana tena leo kuanzia Saa 6:00 mchana kuendelea.
Wakili Lugaziya amesema kuwa wamefikia sehemu nzuri na tayari wameshahoji pande zote mbili za wahusika wa rufaa, mkata rufaa na wakatiwa rufaa.
Wakili Lugaziya amesema Leo wataanzia kwenye kupitia maelezo yao na kisha kutoa maamuzi.
Michael Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika June 29 2014.
Kamati ya Lugaziya ilikutana jana kuanzia Saa 5:00 asubuhi kwenye hoteli ya Courtyard, Upanga, Dar es Salaam kusikiliza rufani moja inayopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba.

0 comments:
Post a Comment