Kombe la dunia Uruguay,Ugiriki mambo safi Ivorycoast kurudi nyumbani
Ugiriki wamefuzu kuingia Raundi ya Pili ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil baada mkwaju wa pelnati Dakika ya 90 kuwapa ushindi wa mabao 2-1 walipocheza na Ivory Coast kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi C.
Mabao yalifungwa na
Georgios Samaras anaechezea Celtic ya Scotland na la kwanza lilifungwa
na Samaris Dakika ya 42 lakini Ivory Coast walisawazisha kwa Bao la Wilfried Bony
na Sare ingeweza kuwafanya wafuze.
Lakini Dakika za Majeruhi, Refa Carlos
Vera wa Ecuador alitoa Penati kwenye Dakika za Majeruhi kwa Rafu
aliyofanyiwa Samaras na Giovanni Sio na kuonekana utata.
Penati hiyo ilifungwa Dakika ya 93 na Samaras.
Mapema jana Uingereza wameiaga Brazil rasmi baada ya
kutoshinda hata Mechi moja ya Fainali za Kombe la Dunia kwa kumaliza
Mechi zao za Kundi D kwa kutoka suluhu Costa Rica ambao kabla ya
Mechi hii walikuwa tayari wameshatinga Raundi ya Pili ya Mtoano.
Kocha Roy Hodgson jana aliipangua
Timu yake na kuwapa nafasi Wachezaji wengi ambao hawakucheza Mechi mbili
za kwanza walizofungwa na Italia 2-1 na Uruguay 2-1.
Italy wametupwa nje ya Kombe la Dunia na
Uruguay baada ya kufungwa Bao 1-0 huku wakicheza wachezaji 10 kufuatia Kadi
Nyekundu kwa Claudio Marchisio kwenye Dakika ya 60.
Mbali ya kufungwa na kupewa Kadi
Nyekundu, hasira kubwa za Italy zipo kwa Refa Marco Rodriguez wa Mexico
kwa kutoona Luis Suarez akimng’ata Meno Beki wa Italy Chiellini.
Bao la ushindi la Uruguay lilifungwa kwa Kichwa na Beki Diego Godin katika Dakika ya 81.
Toka Kundi D, Costa Rica na Uruguay zimesonga Raundi ya Pili ya Mtoano na Italy na England kutupwa nje.
0 comments:
Post a Comment