Pigo kwa Italia Montolivo kukosa kombe la dunia,avunjika.............
Timu ya taifa ya Italia imepata pigo kuelekea kombe la dunia baada ya kiungo wake Riccardo Montolivo kuvunja sehemu ya chini ya goti lake wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Ireland katika dimba la Craven jumamosi hii.
"Ni kitu ambacho tulihofia, kuvunjika. inaweza ikamgharimu zaidi ya mwezi mzima, Riccardo atakuwa nje ya kombe la dunia. Hastahili kuwepo," dakatari wa timu Enrico Castellacci aliliambia kituo cha Tv cha Rai.
Mchezaji huyo wa AC Milan alipata ajali baada ya kukutana uso kwa uso na mlinzi Alex Pearce katika dakika ya 10 na ilimlazimu kutibiwa zaidi ya dakika 5 uwanjani kabla ya kutolewa kwa machela.
Alipelekwa hospitalini na vipimo vya X-ray kuonesha kuwa amevunjika.
Nafasi ya Montolivo ilichukuliwa na Alberto Aquilani, aliyecheza kwa dakika 23 kabla ya kutolewa baada ya kuumizwa pia na timu hizo kutoka 0-0.
Kocha Cesare Prandelii amehuzunishwa na matukio yaliyotokea katika mchezo huo
0 comments:
Post a Comment