Michael Schumacher apata fahamu
Mwendesha magari ya langalanga au F1 Michael Schumacher amepata fahamu.
Michael Schumacher alitoka hospitalini Grenoble na ataendelea kuishi kwa hali yake ya kawaida,familia yake ilisema.Michael Schumacher alipoteza fahamu wakati akiteleza kwenye theluji wakati ajali hiyo ilipotokea.
Schumacher alilazimika kudungwa sindano ya kupoteza fahamu baada ya kupata majeraha mabaya kichwani huko French Alps tarehe 29 Disemba.
Madaktari walichukua hatua hiyo ili kusaidia ubongo uliovimba wa mshindi huyo wa mara saba.
Familia yake iliendelea kwa kushukuru wote waliomtumia jumbe za kumtakia ahueni ya haraka kwa kusema zilimtia moyo,pia waliwashukuru madaktari waliomhudumia alikolazwa katika hospitali ya Grenoble,kusini -mashariki mwa ufaransa.
“Michael ametoka hospitalini CHU Grenoble,
kuanza safari ndefu ya kurudi katika hali yake ya kawaida. Amepata
fahamu,'' Sabine Kehm ambaye ndiye meneja wake alisema katika taaarifa
iliyotolewa kwa niaba ya familia yake.
Wapelelezi katika ajali hiyo wanasema Schumacher alikuwa kwa mwendo wa kasi kama mwenye uzoefu wa mchezo huo wakati wa ajali hiyo Meribel
Schumacher alistaafu kutoka mchezo wa F1 mwaka wa 2012 baada ya kuwa kwa safu hiyo kwa miaka 19. Alishinda taji mbili na Benetton, mnamo mwaka 1994 na 1995, kabla kuelekea Ferrari 1996 na kupendekeza kupata mataji tano kuanzia 2000.
Chanzo;BBC
0 comments:
Post a Comment