Mieleka wanaume watakaopigana kwenye Money in the bank Hawa hapa.
Hatimaye idadi ya watakaoshindania WWE Money in the Bank imekamilika ambapo wanamieleka Roman Reigns, John Cena, Randy Orton, Bray Wyatt, Bingwa wa Marekani Sheamus, Cesaro na Alberto Del Rio watashindana katika mchezo unaohusisha ngazi ili kumpata bingwa mpya wa uzito wa juu duniani.Hapo kabla bingwa anayemiliki mkanda huo Daniel Bryan amejitoa rasmia June 9 baada ya kutopona vema na bado hajakamilisha matibabu yake,mchezo huo ni June 29.
Kwenye historia Cena, Del Rio, Sheamus na Orton wamewahi kuchukua ubingwa huo wa dunia lakiini Reigns, Wyatt na Cesaro hawajawahi kubeba ubingwa huo.
Money in the bank ni mchezo ambao wanamieleka hupigana na kisanduku kufungwa juu na kuning'inia na atakayeshinda ataweka ngazi ili atoe mkanda huo na ndipo atakuwa mshindi .
Kwa matokeo na nini kinaendelea usikose kufuatilia mtandao huu Sports4lifetz
0 comments:
Post a Comment