Tuesday, 17 June 2014

Serikali imeombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii Kilimanjaro

Serikali mkoani Kilimanjaro imeombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii waliopo mkoani hapo ili kuinua tasnia ya filamu sanjari na kusaidia kukuza vipaji vya waigizaji.
Ombi hilo limetolewa na katibu wa chama cha waigizaji na wacheza picha  mkoani Kilimanjaro, Ditram Ngonyani wakati wa mkutano mkuu wa kupitisha katiba ya chama hicho ambayo imewashirikisha viongozi wa chama hicho kutoka katika wilaya zote za mkoa huo.
Ngonyani amesema mara nyingi wasanii wamekuwa wakikosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa serikali waliopo kwenye wilaya hususani maofisa utamaduni jambo ambalo linazorotesha tasnia hiyo na kuiomba serikali kutoa ushirikiano ili kukuza utamaduni katika wilaya husika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho, Ramadhani Msasu, ameiomba serikali kupitia wizara ya habari, tamaduni na michezo kuacha kuwathamini wanamichezo wa mpira wa miguu zaidi na badala yake  maofisa utamaduni wote wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vyama vya sanaa kwani wao ndiyo wanaotangaza utamaduni wa mtanzania.

0 comments:

Post a Comment