Taifa Stars kujitetea kwa Zimbabwe leo,Rwanda na Uganda wafuzu hatua inayofuata
Leo hii juni 1 timu taifa ya Tanzania, Taifa stars itakabiliana na wenyeji wao, Zimbabwe, mjini Harare kwa ajili ya kufuzu mashindano ya AFCON mwaka 2015 kule Morocco.Taifa Stars walioripotiwa kufanyiwa hujuma siku ya ijumaa kwa kufungiwa Hoteli wanayoishi mjini Harare, wanahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kusonga mbele.
Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 walioupata uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam bao lililofungwa na John Bocco.
Ikiwa Taifa Stars itafuzu, Raundi ijayo watacheza na Mshindi kati ya Msumbiji na Sudan ya kusini ambao katika Mechi yao ya kwanza Msumbiji, wakicheza Nyumbani, waliichabanga Sudan mabao 5-0.
Leo pia kuna michezo ambapo Lesotho waliofungwa bao 1-0 ugenini, watawakaribisha wapinzani wao Liberia katika mechi ya marudiano.
Nao Botswana waliotoka suluhu mjini Bujumbura, watawakaribisha Burundi nyumbani kwao.
Congo yenye kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 na Namibia, leo itakuwa nyumbani kulipa kisasi.
Katika mechi nyingine, Benin waliotoka suluhu mechi ya kwanza, watakuwa nyumbani kuvaana na Sao Tome.
Chadi waliofungwa mabao 2-0 na Malawi, leo watakuwa kwenye kibarua kigumu nyumbani kuhitaji kufuta matokoe hayo.
Guinea ya Ikweta iliyofungwa bao 1-0 ugenini, itahitaji ushindi nyumbani katika mechi ya marudiano na Mauritania.
Jana siku ya jumamosi Uganda The Cranes imefanikiwa kusonga hatua inayofuata katika baada ya kufanikiwa kuiondosha Madagascar kwa wastani wa mabao 2-2, lakini Uganda wamenufaika kwa faida ya bao la ugenini.
Rwanda nayo imefuzu baada ya kuifunga Libya mabao 3-0
0 comments:
Post a Comment